Matthew 9:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo huo, mwanamke mmoja, aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakiwa njiani, alikuwepo mwanamke aliyekuwa akitokwa damu kwa miaka kumi na mbili. Alimwendea Yesu kwa nyuma na akagusa sehemu ya chini ya vazi lake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo mwanamke mmoja ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa vazi lake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara akaja mwanamke mwenye kutoka damu miaka 12, akamjia nyuma, akaligusa pindo la nguo yake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kulikuwa mwanamuke mumoja mwenye ugonjwa wa kutokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Yeye akakuja nyuma ya Yesu na kugusa upindo wa nguo yake,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mwanamke, aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka thenashara, alikuja kwa nyuma, akagusa upindo wa vazi lake: