Matthew 9:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaoomboleza,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliendelea kwenda na kiongozi wa Kiyahudi na kuingia nyumbani kwake. Aliwaona watu wapigao muziki kwa ajili ya mazishi pale. Na aliliona kundi la watu waliohuzunika sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaoomboleza,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaoomboleza,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipoingia nyumbani mwa jumbe akawaona wapiga filimbi na kundi la watu, wakiomboleza,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipofika kwa nyumba ya yule mukubwa, akaona wapiga muziki wakiimba nyimbo za kilio nalo kundi la watu wakifanya kelele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, akaona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,