Matthew 9:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akayagusa macho yao na akasema, “Kwa kuwa mnaamini kuwa ninaweza kuwafanya muone, hivyo itatokea.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na mnavyoamini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na itendeke kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowagusa macho akisema: Hayo, mliyoyategemea, na myapate vivyo hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akagusa macho yao, akisema: “Ifanyike kwenu sawa vile munavyoaminia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra akawagusa macho yao, akanena, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.