Matthew 9:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya walimu wa sheria walisikia alichosema Yesu. Wakaambizana wao kwa wao, “Si anamtukana Mungu mtu huyu akasema hivyo!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, waandishi waliokuwako waliposema mioyoni: Huyu anambeza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu walimu wamoja wa Sheria waliokuwa pale wakajisemesha: “Mutu huyu anamutukana Mungu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.