Matthew 9:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawa wawili walipokuwa wanaondoka, baadhi ya watu walimleta mtu mwingine kwa Yesu. Mtu huyu alikuwa haongei kwa sababu alikuwa na pepo ndani yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao walipokuwa wakiondoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao walipotoka, mara wakamletea bubu aliyepagawa na pepo. Naye pepo alipokwisha fukuzwa, yule bubu akaweza kusema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu hao wawili walipokwisha kwenda, wakamuletea Yesu mutu mumoja bubu aliyeshikwa na pepo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta wale walipokuwa wakitoka, wakamletea mtu bubu mwenye pepo.