Matthew 9:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alisafiri akipita katika miji yote na vijiji. Alifundisha katika masinagogi yao na kuwaeleza watu Habari Njema kuhusu ufalme wa Mungu. Aliponya kila aina ya magonjwa na udhaifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme na kuponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Yesu akawa akizunguka mijini mote na vijijini, akawafundisha katika nyumba zao za kuombea, akautangaza Utume mwema wa ufalme, akaponya ugonjwa wote na unyonge wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alizunguka katika miji na vijiji vyote, akiwafundisha watu katika nyumba zao za kuabudia, akiwahubiri Habari Njema ya Ufalme. Aliponyesha magonjwa yote na uzaifu wa kila namna.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.