Matthew 9:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliona watu wengi na kuwahurumia kwa sababu walikuwa wanakandamizwa na hawakuwa na tumaini; kama kondoo bila mchungaji wa kuwaongoza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipoona makutano aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini alipowatazama makundi ya watu akawaonea uchungu, kwani walikuwa wamechoka kwa kuteswa na kutawanyishwa kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipoona kundi la watu, aliwasikilia huruma, kwa maana walikuwa wamesumbuka na kuregea, kama kondoo wasiokuwa na muchungaji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na alipowaona makutano, akawahurumia, kwa maana walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchunga.