Matthew 9:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nataka mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo ndipo mtakapoweza kuona kama kweli ninayo mamlaka hayo ama sina.” Kwa hiyo Yesu akamwambia mtu yule aliyepooza, “Nitalithibitishaje hili kwako? Ninakwambia hivi, ‘Inuka! Beba kitanda chako uende nyumbani!’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako na uende nyumbani kwako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini, ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Inuka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kusudi mpate kujua, ya kuwa Mwana wa mtu ana nguvu ya kuondoa makosa nchini, - basi, akamwambia mwenye kupooza: Inuka, jitwishe kitanda chako, uende nyumbani kwako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ninataka mujue kwamba Mwana wa Mutu yuko na mamlaka ya kusamehe zambi hapa katika dunia.” Kwa hiyo akamwambia yule mutu mwenye kupooza: “Simama, utwae kipoyi chako na uende kwako.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini illi mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako.