Matthew 9:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati wa watu walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu aliyekuwa amewakabidhi wanadamu mamlaka kama haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu walipoliona tukio hili wakashangaa. Wakamsifu Mungu kwa kuwapa watu mamlaka hii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama hii kwa wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama haya kwa wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini makundi ya watu walipoyaona wakaogopa, wakamtukuza Mungu aliyewapa watu nguvu kama hizo.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walipoona jambo hilo wakaogopa na kumusifu Mungu aliyewapa watu mamlaka ya namna ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.