Micah 1:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaoishi Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hata katika lango la Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema; Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa Bwana, Umefika mpaka lango la Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa BWANA, hata katika lango la Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa bwana, hata katika lango la Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema; Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA, Yamefika katika lango la Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaao Maroti (Uchungu) wanaona uchungu kwa ajili ya mema yao, kwani mabaya yameyashukia malango ya Yerusalemu toka kwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema; Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa BWANA, Umefika mpaka lango la Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa Maroti wanangojea musaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yanakuja kutoka kwa Yawe karibu kabisa na mulango wa Yerusalema.