Micah 1:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki; Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki; Utukufu wa Israeli utafika Adulamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mkaao Maresa (Wenyeji) nitawaletea mwenyeji wa kweli, utukufu wa Isiraeli utajiendea mpaka Adulamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki; Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi wakaaji wa Maresa, Mungu atawaletea tena adui atakayewateka. Waongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia ndani ya pango kule Adulamu.