Micah 1:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yanayotiririka kasi kwenye mteremko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mtelemko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, milima itakapoyeyuka chini yake, nayo mabonde yataatuka nyufa; itayeyuka kama nta motoni, iwe kama maji yaporomokayo magengeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Milima itayeyuka chini ya miguu yake, kama inta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama vile maji yanayoporomoka kwenye muteremuko.