Micah 1:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya yote yatatukia kwa sababu ya makosa ya wazawa wa Yakobo, kwa sababu ya dhambi za wazawa wa Israeli. Je, uhalifu wa Yakobo waonekana wapi? Katika mji wake mkuu Samaria! Je, uhalifu wa Yuda waonekana wapi? Katika Yerusalemu kwenyewe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia ni nini? Je, sio Yerusalemu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya yote yatatukia kwa sababu ya makosa ya wazawa wa Yakobo, kwa sababu ya dhambi za wazawa wa Israeli. Je, uhalifu wa Yakobo waonekana wapi? Katika mji wake mkuu Samaria! Je, uhalifu wa Yuda waonekana wapi? Katika Yerusalemu kwenyewe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya yote yatatukia kwa sababu ya makosa ya wazawa wa Yakobo, kwa sababu ya dhambi za wazawa wa Israeli. Je, uhalifu wa Yakobo waonekana wapi? Katika mji wake mkuu Samaria! Je, uhalifu wa Yuda waonekana wapi? Katika Yerusalemu kwenyewe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote yatakuja kwa ajili ya upotovu wa Yakobo, na kwa ajili ya makosa yao walio mlango wa Isiraeli. Upotovu wa Yakobo ndio nini? Sio ule wa Samaria? Napo pa kutambikia vilimani ndipo wapi? Sipo Yerusalemu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya yote yatatukia kwa sababu ya makosa ya wazao wa Yakobo, kwa sababu ya zambi za wazao wa Israeli. Kosa la Yakobo linaonekana wapi? Katika muji wake mukubwa Samaria! Kosa la Yuda linaonekana wapi? Katika Yerusalema kwenyewe!