Micah 2:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi: “Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui. Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu; watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi, na wasio na fikira zozote za vita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hizi watu wangu wameinuka kama adui. Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita pasipo kujali, kama watu warudio kutoka vitani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi: “Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui. Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu; watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi, na wasio na fikira zozote za vita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hizi watu wangu wameinuka kama adui. Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita pasipo kujali, kama watu warudio kutoka vitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hizi watu wangu wameinuka kama adui. Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita pasipo kujali, kama watu warudio kutoka vitani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mnawapokonya joho lililo juu ya nguo za hao wapitao salama bila kutarajia vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi: “Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui. Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu; watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi, na wasio na fikira zozote za vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tangu kale mmewainukia walio ukoo wangu, kama ni adui zenu; wapitao pasipo mawazo mabaya mwawavua kanzu za juu na mavazi ya ndani, kama ni mateka ya vitani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe anawaambia ninyi hivi: Munawatendea watu wangu kama adui. Munawanyanganya watu watulivu nguo zao; watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi, na wasiokuwa na mafikiri yoyote ya vita.