Micah 3:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea Mwenyezi Mungu na kusema, “Je, Mwenyezi Mungu si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea Bwana, na kusema, Je! Hayupo Bwana katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea BWANA na kusema, “Je, BWANA si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea bwana na kusema, “Je, bwana si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wao hukata mashauri kwa kupenyezewa mali, nao watambikaji wao hufundisha kulipwa, nao wafumbuaji wao hufumbua kwa kupata fedha, tena hujiegemezea kwake Bwana na kusema: Je? Bwana hayuko kwetu katikati? Hakuna kibaya kitakachotupata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamuzi wanahukumu kwa kupewa kutuliro, makuhani wake wanafundisha kwa kupata malipo, manabii wanatabiri kwa kupata feza. Hata hivyo wanajidai kumutegemea Yawe, wakisema: Yawe, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na hasara yoyote!