Micah 3:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, mtu akiwalisha, wanatangaza ‘amani’; kama hakufanya hivyo, wanaandaa kupigana vita dhidi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, mtu akiwalisha, wanatangaza ‘amani’; kama hakufanya hivyo, wanaandaa kupigana vita dhidi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, mtu akiwalisha, wanatangaza ‘amani’; kama hakufanya hivyo, wanaandaa kupigana vita dhidi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya wafumbuaji wanaowapoteza walio ukoo wangu, ndio wanaotangaza kwamba: Tengemaneni tu! wakipata vya kutafuna kwa meno yao, lakini mtu asipowapa vya kutia vinywani mwao, humpatia vita vya watakatifu
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi juu ya manabii wanaowapotosha watu wake, manabii ambao wanatabiri amani wakipewa kitu, lakini wanawatishia watu kwa vita wasipopewa kitu: