Micah 3:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mimi nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa Mwenyezi Mungu, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa BWANA, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa bwana, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi nimejaa nguvu, nilizopewa na Roho ya Bwana, nikapewa kumaliza mashauri kwa uwezo wa kushinda, nipate kuwatangazia wa Yakobo mapotovu yao nao Waisiraeli makosa yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Yawe; nimejaliwa kufuata sheria ya Mungu na kuwa na uwezo niwatangazie wazao wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli zambi yao.