Micah 4:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Mwenyezi Mungu utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote; utainuliwa juu ya vilima, na watu wa mataifa watamiminika humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la BWANA utaimarishwa na kuwa mkuu kuliko milima yote; utainuliwa juu ya vilima na mataifa yatamiminika humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la bwana utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote; utainuliwa juu ya vilima, na watu wa mataifa watamiminika humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwisho wa siku utakapotimia, mlima wenye Nyumba ya Bwana utakuwa umeshikizwa na nguvu, uwe wa kwanza wa milima, uende juu kuliko vilima vingine; ndiko, makabila ya watu watakakokimbilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutakuja wakati ambapo mulima wa nyumba ya Yawe utakuwa mukubwa kuliko milima yote. Utanyanyuliwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watakimbilia kule,