Micah 4:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi watu wa Siyoni, lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua! Maana sasa mtaondoka katika mji huu mwende kukaa nyikani, mtakwenda mpaka Babuloni. Lakini huko, mtaokolewa. Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gaagaa kwa uchungu, ee Binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa, kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji ukapige kambi uwanjani. Utaenda Babeli; huko utaokolewa. Huko Mwenyezi Mungu atakukomboa kutoka mikononi mwa adui zako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa katika mikono ya adui zako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watu wa Siyoni, lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua! Maana sasa mtaondoka katika mji huu mwende kukaa nyikani, mtakwenda mpaka Babuloni. Lakini huko, mtaokolewa. Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gaagaa kwa utungu, Ee Binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji ukapige kambi uwanjani. Utakwenda Babeli; huko utaokolewa. Huko BWANA atakukomboa kutoka mikononi mwa adui zako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji ukapige kambi uwanjani. Utakwenda Babeli; huko utaokolewa. Huko bwana atakukomboa kutoka mikononi mwa adui zako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwe na uchungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko BWANA atakakokukomboa katika mikono ya adui zako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi watu wa Siyoni, lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua! Maana sasa mtaondoka katika mji huu mwende kukaa nyikani, mtakwenda mpaka Babuloni. Lakini huko, mtaokolewa. Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jipinde na kupiga kite kama mwanamke anayezaa, binti Sioni! Kwani sasa huna budi kutoka mjini, ukae porini, mpaka ufike Babeli; huko ndiko, Bwana atakakokuponya akikukomboa mikononi mwa adui zako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko BWANA atakakokukomboa katika mikono ya adui zako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu wa Sayuni, mulie na kugaagaa kama mwanamuke anayezaa! Maana sasa mutaondoka katika muji huu muende kukaa katika mbuga, mutakwenda mpaka Babeli. Lakini kule, mutaokolewa. Kule Yawe atawakomboa toka katika makucha ya waadui zenu.