Micah 4:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wao hawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Mungu wala hawaelewi mpango wake: Kwamba amewakusanya pamoja, kama miganda mahali pa kupuria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hawayajui mawazo ya Mwenyezi Mungu; hawauelewi mpango wake, yeye awakusanyaye kama miganda kwenye sakafu ya kupuria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wao hawayajui mawazo ya Bwana, wala hawafahamu shauri lake; kwa maana amewakusanya kama miganda sakafuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wao hawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Mungu wala hawaelewi mpango wake: kwamba amewakusanya pamoja, kama miganda mahali pa kupuria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hawayajui mawazo ya BWANA; hawauelewi mpango wake, yeye awakusanyaye kama miganda kwenye sakafu ya kupuria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hawayajui mawazo ya bwana; hawauelewi mpango wake, yeye awakusanyaye kama miganda kwenye sakafu ya kupuria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wao hawayajui mawazo ya BWANA, wala hawafahamu shauri lake; kwamba amewakusanya kama miganda mahali pa kupuria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wao hawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Mungu wala hawaelewi mpango wake: Kwamba amewakusanya pamoja, kama miganda mahali pa kupuria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wao hawayajui mawazo ya Bwana, wala hawalitambui shauri lake, ya kuwa ni yeye aliyewakusanya kama miganda penye kupuria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wao hawayajui mawazo ya BWANA, wala hawafahamu shauri lake; kwa maana amewakusanya kama miganda sakafuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wao hawafahamu mawazo ya Yawe wala hawaelewi mupango wake: kwamba amewakusanya pamoja, kama miganda pahali pa kupepetea.