Micah 4:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Inuka upure, ee Binti Sayuni, kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; nitakupa kwato za shaba na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Mwenyezi Mungu, utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda-ponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa Bwana, na mali zao kwa Bwana wa dunia yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Inuka upure, Ee Binti Sayuni, kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; nitakupa kwato za shaba na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa BWANA, utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Inuka upure, ee Binti Sayuni, kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; nitakupa kwato za shaba na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa bwana, utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inuka, binti Sioni, uwapure! Kwani pembe zako nitazigeuza kuwa chuma nayo kwato zako kuwa shaba, upate kuponda makabila mengi, umtolee Bwana mapato yao, yawe yake, nazo mali zao, ziwe zake yeye aliye Bwana wa nchi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda-ponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema: Enyi watu wa Sayuni, musimame muwakanyagekanyage! Nitawapatia nguvu kama ngombe dume mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mutawasaga watu wa mataifa mengi; mutanitolea mimi mapato yao, mutanitolea mali zao mimi Bwana wa dunia yote.