Micah 4:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni kwenye mlima wa Mwenyezi Mungu, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Torati itatoka Sayuni, neno la Mwenyezi Mungu litatoka Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njoni, twendeni mlimani kwa BWANA, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tutembee katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la BWANA litatoka Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la bwana litatoka Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njooni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wamizimu wengi watakwenda huko wakisema: Njoni, tupande mlimani kwa Bwana kwenye Nyumba ya Mungu wa Yakobo! Atufundishe, njia zake zilivyo, tupate kwenda na kuifuata mikondo yake! Kwani Maonyo yatatoka Sioni, namo Yerusalemu mtatoka Neno lake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mataifa mengi yataufikia na kusema: Tuende juu kwenye mulima wa Yawe, tuende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, kusudi atufundishe njia zake, nasi tuzifuate. Maana sheria itatoka kule Sayuni; na neno la Yawe kule Yerusalema.