Micah 4:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atahukumu kati ya mataifa mengi, na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atahukumu kati ya mataifa mengi na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe ya kulimia na mikuki yao kuwa miundu ya kukatia matawi. Taifa halitachukua upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atahukumu kati ya mataifa mengi, na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, atakapoamulia makabila mengi na kuwapatiliza wamizimu wenye nguvu wakaao mbali; nao watazifua panga zao kuwa majembe, hata mikuki yao kuwa miundu, kwani hakuna taifa tena litakalochomolea jingine panga, wala hawatajifundisha tena mapigano ya vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu atatoa hukumu kati ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa visu vya kuvuna. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.