Micah 4:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe kilima cha Yerusalemu, wewe ngome ya Siyoni, ambamo Mungu anafanya ulinzi juu ya watu wake, kama mchungaji juu ya kondoo wake; wewe utakuwa tena mji maarufu kama hapo awali, Yerusalemu utakuwa tena mji mkuu wa mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwako wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi, ee ngome ya Binti Sayuni, milki ya awali itarudishwa kwako, ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe kilima cha Yerusalemu, wewe ngome ya Siyoni, ambamo Mungu anafanya ulinzi juu ya watu wake, kama mchungaji juu ya kondoo wake; wewe utakuwa tena mji maarufu kama hapo awali, Yerusalemu utakuwa tena mji mkuu wa mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kuhusu wewe, Ee mnara wa ulinzi wa kundi, Ee ngome ya Binti Sayuni, milki ya awali itarudishwa kwako, ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi, ee ngome ya Binti Sayuni, milki ya awali itarudishwa kwako, ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe kilima cha Yerusalemu, wewe ngome ya Siyoni, ambamo Mungu anafanya ulinzi juu ya watu wake, kama mchungaji juu ya kondoo wake; wewe utakuwa tena mji maarufu kama hapo awali, Yerusalemu utakuwa tena mji mkuu wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe mnara wa kulindia makundi, wewe kilima cha binti Sioni, kwako wewe utarudi tena, ukufikie, ule utawalaji wa kwanza, ndio ufalme wa binti Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe kilima cha Yerusalema, wewe munara wa Sayuni, ambamo Mungu anafanya ulinzi juu ya watu wake, kama muchungaji juu ya kondoo wake, wewe utakuwa tena muji wenye mamlaka sawa zamani. Yerusalema utakuwa tena muji mukubwa wa mufalme.