Micah 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumuikeni mkajikusanye enyi watu wa Yerusalemu; mkisema: “Tumezingirwa, tumesongwa; naye kiongozi wa Israeli wanampiga shavuni kwa fimbo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema, “Lakini wewe Bethlehemu katika Efratha, wewe ni mdogo tu kati ya jamii za Yuda, lakini kwako kutatoka mtawala atakayetawala juu ya Israeli kwa niaba yangu. Asili yake ni ya zama za kale.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Panga majeshi yako, Ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumuikeni mkajikusanye enyi watu wa Yerusalemu; mkisema: “Tumezingirwa, tumesongwa; naye kiongozi wa Israeli wanampiga shavuni kwa fimbo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Wewe Beti-Lehemu wa Efurata, ijapo uwe mdogo katika miji yenye maelfu ya Yuda, mwako ndimo, atakamonitokea yeye atakayekuwa mtawala Waisiraeli; matokeo yake ni ya siku nyingi za mbele, kweli ni ya siku za kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Lakini wewe Betelehemu katika Efurata, wewe ni mudogo tu kati ya ukoo wa Yuda, lakini kwako kutanitokea mutawala atakayetawala juu ya Israeli. Asili yake ni ya zamani sana.