Micah 5:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mtawala atawachunga watu wake kwa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, kwa fahari yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wake. Watu wake wataishi kwa usalama, maana atakuwa mkuu mpaka miisho ya dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya Mwenyezi Mungu, katika utukufu wa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye ndiye atakayeleta amani. Waashuru wakivamia nchi yetu, na kuupenya ulinzi wetu, tutapeleka walinzi wawakabili, naam, tutawapeleka viongozi wetu kwa wingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya BWANA, katika utukufu wa jina la BWANA Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya bwana, katika utukufu wa jina la bwana Mwenyezi Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mtawala atawachunga watu wake kwa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, kwa fahari yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wake. Watu wake wataishi kwa usalama, maana atakuwa mkuu mpaka miisho ya dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye yeye atakuwa utengemano wetu.* Kama Waasuri wataingia katika nchi yetu, wakanyage namo majumbani mwetu, tutaweka wachungaji wetu saba, wawazuie, pamoja na watu wanane wa kifalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ndiye atakayeleta amani. Waasuria wakishambulia inchi yetu, na kuingia katika nyumba zetu nzuri, tutatuma walinzi wetu wapigane nao, tutawapeleka waongozi wetu kwa wingi.