Micah 5:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa silaha zao wataitawala nchi ya Ashuru, na kuimiliki nchi ya Nimrodi. Watatuokoa mikononi mwa Waashuru, watakapowasili mipakani mwa nchi yetu na kuanza kuivamia nchi yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, nchi ya Nimrodi kwa upanga. Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru atakapoivamia nchi yetu na kuingia katika mipaka yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai wameenea miongoni mwa mataifa mengi, watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao, kama manyunyu yaangukayo penye nyasi ambayo hayasababishwi na mtu wala kumtegemea binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, nchi ya Nimrodi kwa upanga. Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru atakapoivamia nchi yetu na kuingia katika mipaka yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, nchi ya Nimrodi kwa upanga. Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru atakapoivamia nchi yetu na kuingia katika mipaka yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa silaha zao wataitawala nchi ya Ashuru, na kuimiliki nchi ya Nimrodi. Watatuokoa mikononi mwa Waashuru, watakapowasili mipakani mwa nchi yetu na kuanza kuivamia nchi yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao masao ya Isiraeli watakuwa kati ya makabila mengi kama umande utokao kwa Bwana, au kama manyunyu yanyeayo majani yasiyomngojea mtu, yasiyokalii wana wa watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Yakobo watakaobaki wazima wataenea kati ya mataifa mengi, watakuwa kama umande unaotoka kwa Yawe, kama manyunyu yanayoanguka kwenye majani ambayo hayasababishwi na mutu wala kumutegemea mwanadamu.