Micah 5:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai wameenea miongoni mwa mataifa mengi, watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao, kama manyunyu yaangukayo penye nyasi ambayo hayasababishwi na mtu wala kumtegemea binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai, wameenea miongoni mwa mataifa na watu wengi watakuwa na nguvu kubwa kama simba kati ya wanyama wa porini, kama mwanasimba miongoni mwa makundi ya kondoo, ambaye kila mahali apitapo, huyarukia na kuyararua mawindo yake, asiwepo mtu yeyote wa kuyaokoa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa BWANA, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa bwana, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai wameenea miongoni mwa mataifa mengi, watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao, kama manyunyu yaangukayo penye nyasi ambayo hayasababishwi na mtu wala kumtegemea binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli masao ya Yakobo watakuwa kwa wamizimu kati ya makabila mengi, kama simba alivyo katika nyama wa porini, au kama mwana wa simba alivyo katika makundi ya kondoo, akiwapita huwakanyaga pamoja na kuwararua, asipatikane mponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Yakobo watakaobaki wazima, wataenea kati ya mataifa na watu wengi watakuwa na nguvu kubwa kama simba kati ya nyama wa pori, kama simba mukali kati ya makundi ya kondoo, ambaye kila pahali anapopita, anarukia na kurarua nyama, na hakuna mutu yeyote wa kuiokoa.