Micah 6:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Mwenyezi Mungu, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikieni, enyi milima, mateto ya Bwana, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana Bwana ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikilizeni, Ee milima, mashtaka ya BWANA, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa BWANA ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya bwana, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa bwana ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi milima, yasikieni masuto ya Bwana! Yasikieni nanyi miamba mlio misingi ya nchi! Kwani Bwana ana shauri nao walio ukoo wake, hana budi kuumbuana na Waisiraeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikieni, enyi milima, mateto ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize mashitaki ya Yawe, enyi milima, musikilize enyi misingi imara ya dunia! Yawe yuko na maneno juu ya watu wake. Yeye atatoa mashitaki juu ya Waisraeli.