Micah 6:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi watu wangu, kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu, na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu. Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali. Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu alivyofanya shauri na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu hadi Gilgali, ili mfahamu matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watu wangu, kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu, na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu. Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali. Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu alivyofanya shauri na kile Balamu mwana wa Beori alichojibu. Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali, ili mfahamu matendo ya haki ya BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu alivyofanya shauri na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali, ili mfahamu matendo ya haki ya bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi watu wangu, kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu, na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu. Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali. Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlio ukoo wangu, yakumbukeni, Balaka, mfalme wa Moabu, aliyowawazia, nayo Bileamu, mwana wa Beori, aliyomjibu! Yakumbukeni nayo yaliyofanyika toka Sitimu mpaka Gilgali, mpate kujua, ya kuwa Bwana ni mwongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu wangu, mukumbuke mipango mibaya ya Balaki mufalme wa Moabu, na jinsi Balama mwana wa Beori alivyomujibu. Mukumbuke yaliyotukia katika njia kati ya Sitimu na Gilgali. Mukumbuke, mutambue matendo yangu ya kuwaokoa!