Micah 6:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwa nikimtolea maelfu ya kondoo madume, au mito elfu na elfu ya mafuta? Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, naam, mtoto wangu kwa ajili ya dhambi yangu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Mwenyezi Mungu atafurahishwa na kondoo dume elfu, au mito elfu kumi ya mafuta? Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, mtoto wangu mwenyewe kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwa nikimtolea maelfu ya kondoo madume, au mito elfu na elfu ya mafuta? Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, naam, mtoto wangu kwa ajili ya dhambi yangu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, BWANA atafurahishwa na kondoo dume elfu, au mito elfu kumi ya mafuta? Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, mtoto wangu mwenyewe kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu, au mito elfu kumi ya mafuta? Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, mtoto wangu mwenyewe kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! BWANA atapendezwa na maelfu ya kondoo dume, au na makumi elfu ya mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzawa wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwa nikimtolea maelfu ya kondoo madume, au mito elfu na elfu ya mafuta? Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, naam, mtoto wangu kwa ajili ya dhambi yangu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Bwana atapendezwa na maelfu ya madume ya kondoo? Au atapendezwa na maelfu kumi ya vijito vya mafuta? Au nimpe mwanangu wa kwanza, awe ng'ombe ya tambiko ya kuondolea mapotovu yangu? Je? Zao la tumbo langu liyalipe makosa ya roho yangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atapendezwa nikimutolea maelfu ya kondoo dume, au mito elfu na elfu ya mafuta? Nimutolee muzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, mutoto wangu wa kwanza kwa ajili ya zambi yangu?