Micah 7:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wangu! Hali ilivyo ni kama baada ya mavuno; hakuna tini za mwanzoni ninazotamani. Ni kama wakati wa kuchuma zabibu hakuna hata shada moja la zabibu la kula!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Taabu gani hii niliyo nayo! Nimefanana na yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mizabibu; hakuna kishada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa hari, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wangu! Hali ilivyo ni kama baada ya mavuno; hakuna tini za mwanzoni ninazotamani. Ni kama wakati wa kuchuma zabibu hakuna hata shada moja la zabibu la kula!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Taabu gani hii niliyo nayo! Nimefanana na yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mizabibu; hakuna kishada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Taabu gani hii niliyo nayo! Nimefanana na yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mizabibu; hakuna kishada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa joto, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wangu! Hali ilivyo ni kama baada ya mavuno; hakuna tini za mwanzoni ninazotamani. Ni kama wakati wa kuchuma zabibu hakuna hata shada moja la zabibu la kula!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yamenipata! Kwani yamenijia mambo yapatikanayo penye mwisho wa machumo ya matunda, siku za kiangazi zikitimia, au watu wakiokotezaokoteza zabibu: hakuna kichala cha zabibu za kula wala kuyu tu, roho yangu inazozitunukia sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa hari, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole wangu! Mimi ninakuwa kama muvunaji kisha wakati wa mavuno; hakuna tini za kwanzakwanza ninazotamani. Ni kama wakati wa kuchuma zabibu: hakuna hata fungu moja la zabibu la kula!