Micah 7:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vinavyotambaa ardhini. Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; watamgeukia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa hofu nao watakuogopa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa Bwana, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; watamgeukia BWANA Mungu wetu kwa hofu nao watakuogopa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; watamgeukia bwana Mwenyezi Mungu wetu kwa hofu nao watakuogopa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watalamba mavumbi kama nyoka, kama wadudu watambaao chini watatoka mafichoni mwao na kutetemeka, wamjie Bwana Mungu wetu kwa kutishika, nawe wewe watakuogopa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watatambaa katika mavumbi kama nyoka, kama viumbe vinavyotambaa. Watatoka katika makimbilio yao wakitetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia Yawe, Mungu wetu, kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.