Micah 7:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote ni mabingwa wa kutenda maovu; viongozi na mahakimu hutaka rushwa. Wakubwa huonesha wazi nia zao mbaya, na kufanya hila kuzitekeleza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, mtawala anadai zawadi, hakimu anapokea rushwa, wenye nguvu wanaamuru wanachotaka: wote wanapanga njama pamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mikono yao inayashika mabaya wayatende kwa bidii; mtu mkuu aomba rushwa, kadhi yu tayari kuipokea; mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote ni mabingwa wa kutenda maovu; viongozi na mahakimu hutaka rushwa. Wakubwa huonesha wazi nia zao mbaya, na kufanya hila kuzitekeleza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, mtawala anadai zawadi, hakimu anapokea rushwa, wenye nguvu wanaamuru wanachotaka: wote wanafanya shauri baya pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, mtawala anadai zawadi, hakimu anapokea rushwa, wenye nguvu wanaamuru wanachotaka: wote wanafanya shauri baya pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote ni mabingwa wa kutenda maovu; viongozi na mahakimu hutaka rushwa. Wakubwa huonesha wazi nia zao mbaya, na kufanya hila kuzitekeleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ni kufanya mabaya, mikono yote miwili iko tayari, yamalizike vema. Mkuu ayatakayo, mwenye kukata mashauri huyafanya akipenyezewa mali; mwenye nguvu akiyasema, roho yake inayoyatamani, basi, yayo hayo wanayafunganyafunganya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mikono yao inayashika mabaya wayatende kwa bidii; mtu mkuu aomba rushwa, kadhi yu tayari kuipokea; mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote ni wafundi wa kutenda maovu; waongozi na waamuzi wanaomba kituliro. Wakubwa wanaonyesha wazi nia zao mbaya, nao wanashirikiana pamoja kwa kuzitimiza.