Micah 7:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, hadi atakapotetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitaivumilia ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea teto langu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya BWANA, mpaka atakaponitetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya bwana, mpaka atakaponitetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makali yake Bwana nitayavumilia, kwani nimemkosea: mwisho atanigombea magomvi yangu, anikatie shauri lililo sawa, atanitoa na kuniweka mwangani, nipate kuuona wongofu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea teto langu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa vile nimemukosea Yawe, nitavumilia kasirani yake, mpaka atakapotetea maneno yangu na kunijalia haki yangu. Atanileta inje kwenye mwangaza, nami nitaona akisimamisha haki.