Nahum 1:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, Ee Yuda, sitakutesa tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ingawa wakae na kutulia kwa kuwa wengi hivyo, watakatwa, watoweke. Lakini wewe, kama nimekunyenyekeza, sitakunyenyekeza tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Ingawa Waasuria ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa ninyi watu wangu, sitawatesa tena zaidi.