Nahum 1:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ndiyo amri Mwenyezi Mungu aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kusubu zilizopo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo amri BWANA aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo amri bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa ajili yako (Asuri) Bwana ameagiza, wenye jina lako wasipewe tena kuzaa, namo nyumbani mwa mungu wako nitavitowesha vinyago vya kuchonga navyo vya kuyeyusha, nawe nitakuchimbia kaburi lako, kwani umeonekana kuwa mwepesi zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe ameamuru hivi juu ya Ninawe: Hautapata wazao kwa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za chuma chenye kuyeyushwa, nitazivunjavunja katika nyumba za miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe haufai kwa kitu chochote.