Nahum 1:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, huwaka ghadhabu juu ya adui zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi juu ya watesi wake, naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, huwaka ghadhabu juu ya adui zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; BWANA hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. BWANA hulipiza kisasi juu ya watesi wake, naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake, naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, huwaka ghadhabu juu ya adui zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ni Mungu mwenye wivu alipizaye; kwani Bwana ni mlipizaji mwenye makali, Bwana huwalipiza wapingani wake, nao wachukivu wake huwashikia makali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe ni Mungu mwenye wivu, anayelipiza kisasi; Yawe analipiza kisasi na ni mwenye kasirani; Yawe analipiza kisasi kwa wapinzani wake, kasirani yake inawaka juu ya waadui zake.