Nahum 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, Mwenyezi Mungu hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, BWANA hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, bwana hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ni mvumilivu, mwenye nguvu kuu, lakini aliye mkosaji hamwachilii, asimpatilize. Njia yake Bwana imo katika kimbunga na katika upepo mkali, nayo mawingu ndiyo mavumbi ya miguu yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Yawe hatawaachilia wenye makosa hata kidogo. Yawe anapopita, upepo mukali na zoruba vinatokea; mawingu ni mavumbi yanayonyanyuliwa na miguu yake.