Nahum 2:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Liko wapi sasa pango la simba, ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walienda, na wana simba pia, bila kuogopa chochote?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Liko wapi sasa pango la simba, mahali ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walikwenda na ambapo wana simba walikwenda bila kuogopa cho chote?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Liko wapi sasa pango la simba, mahali ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walikwenda na ambapo wana simba walikwenda bila kuogopa chochote?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba dume na simba jike na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa kuwa mioyo imeyeyuka, uko uchi na utupu na ukiwa, nayo magoti yanagotanagotana, viuno vyote vinatetemeka, nazo nyuso zao wote zimewapoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muji wa Ninawe ni maangamizi matupu na uharibifu! Watu wamekufa moyo, magoti yanagongana, nguvu zimewaishia, nyuso zimebadilika!