Nahum 2:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anatangaza, “Mimi ni kinyume na ninyi. Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto, na upanga utakula wana simba wako. Sitawaachia mawindo juu ya nchi. Sauti za wajumbe wako hazitasikika tena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote anatangaza, “Mimi ni kinyume na ninyi. Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto, na upanga utakula wana simba wako. Sitawaachia mawindo juu ya nchi. Sauti za wajumbe wako hazitasikika tena.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote anatangaza, “Mimi ni kinyume na ninyi. Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto, na upanga utakula wana simba wako. Sitawaachia mawindo juu ya nchi. Sauti za wajumbe wako hazitasikika tena.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo wapi, simba waliporarua nyama, mpaka watoto wao washibe? Ndipo wapi, walipoona nyama wa kuwapatia nao wake zao? Ndipo wapi, walipojaza mapango yao nyama, waliowararua? Yako wapi mashimo yao nyama wao hao, waliowararua?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akiwakamatia simba dike nyama zao; ameyajaza mapango yake na nyama, na makao yake vipande vya nyama.