Nahum 3:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wa mji unaomwaga damu, uliojaa uongo, uliojaa nyara, na usiokosa mateka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wa mji umwagao damu, uliojaa uongo, umejaa nyara, usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wa mji umwagao damu, uliojaa uongo, umejaa nyara, usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yataupata huo mji wenye damu! Wote mzima umejaa uwongo na ukorofi! Haukuacha kupokonya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi; mateka hayaondoki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole wako muji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mutupu na wizi tele, haukomi hata kidogo kunyanganya.