Nahum 3:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako kama makundi ya nzige wanaotua kwenye kuta wakati wa siku ya baridi; lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna anayejua wanakoenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako ni kama makundi ya nzige watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi: lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna ajuaye waendako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako ni kama makundi ya nzige watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi: lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna ajuaye waendako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, wala hapana ajuaye walikokwenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wako wa serikali wanafanana na nzige, nao wakuu wako wa askari wanafanana na makundi ya nyenze: siku za baridi huja kulala kutani, lakini jua likitoka, hujiendea kwa kuruka, tena mahali, walipokwenda, hapajulikani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wako ni kama mapanzi, majemadari wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua linapotokea, wanaruka, wala hakuna anayejua nafasi walipokwenda.