Nahum 3:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anasema, “Mimi ni kinyume na ninyi. Nitafunika uso wako kwa gauni lako. Nitaonesha mataifa uchi wako na falme aibu yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote anasema, “Mimi ni kinyume na ninyi. Nitafunika uso wako kwa gauni lako. Nitaonyesha mataifa uchi wako na falme aibu yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote anasema, “Mimi ni kinyume na ninyi. Nitafunika uso wako kwa gauni lako. Nitaonyesha mataifa uchi wako na falme aibu yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Utaniona, nikikujia, nizifunue nguo zako ndefu nikizipandisha mpaka usoni kwako, nionyeshe mataifa uchi wako, nao walio wa kifalme niwaonyeshe yako yenye soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Yawe wa majeshi ninasema nitakushambulia; nitapandisha nguo yako mpaka kwenye kichwa, niyaache mataifa yauone uchi wako, falme zitaona haya yako.