Nehemiah 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni nao wamerudi kwenye lile jimbo wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaniambia: Yale masao ya watu waliosalia kule jimboni, wenzao walipohamishwa, wamo katika mabaya mengi yawatiayo soni: boma la Yerusalemu lingaliko limebomolewa, nayo malango yake yako vivyo hivyo, yalivyoteketezwa kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao wakaniambia: “Wayuda walioponyoka na kubaki katika jimbo lile, wako katika taabu nao wanazarauliwa. Ukuta wa Yerusalema umebomolewa na milango yake imeteketezwa.”