Nehemiah 10:29 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tunaungana na ndugu zetu, wakuu wetu, katika kula kiapo na kwamba tukivunja kiapo hiki tutaapizwa, na twaapa kuwa tutaishi kwa kufuata sheria ya Mungu ambayo aliitoa kwa njia ya Mose, mtumishi wake. Tena tutatii yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anatuamuru, na kuwa tutashika maagizo yake na kufuata masharti yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Torati ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Musa mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za Mwenyezi Mungu, Bwana wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za Bwana, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tunaungana na ndugu zetu, wakuu wetu, katika kula kiapo na kwamba tukivunja kiapo hiki tutaapizwa, na twaapa kuwa tutaishi kwa kufuata sheria ya Mungu ambayo aliitoa kwa njia ya Mose, mtumishi wake. Tena tutatii yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anatuamuru, na kuwa tutashika maagizo yake na kufuata masharti yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi hawa wote wakajiunga na ndugu zao na wakuu wao, wakajifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za BWANA, Bwana wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Torati ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Musa mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za bwana, Bwana wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tunaungana na ndugu zetu, wakuu wetu, katika kula kiapo na kwamba tukivunja kiapo hiki tutaapizwa, na twaapa kuwa tutaishi kwa kufuata sheria ya Mungu ambayo aliitoa kwa njia ya Mose, mtumishi wake. Tena tutatii yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anatuamuru, na kuwa tutashika maagizo yake na kufuata masharti yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakawafuata ndugu zao watukufu wakijiapiza na kuapa kwamba: Tuendelee na kuyafuata Maonyo ya Mungu yaliyotolewa mkononi mwa Mose, mtumishi wake Mungu, tena tuyashike na kuyafanya maagizo yote na maamuzi yake na maongozi yake Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake;