Nehemiah 10:34 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi sote, watu wote, makuhani na Walawi tutapiga kura kila mwaka ili kuchagua ukoo utakaoleta kuni za kuteketeza tambiko madhabahuni pa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama sheria ilivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa Bwana, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi sote, watu wote, makuhani na Walawi tutapiga kura kila mwaka ili kuchagua ukoo utakaoleta kuni za kuteketeza tambiko madhabahuni pa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama sheria ilivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya BWANA Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya bwana Mwenyezi Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Torati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa BWANA, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi sote, watu wote, makuhani na Walawi tutapiga kura kila mwaka ili kuchagua ukoo utakaoleta kuni za kuteketeza tambiko madhabahuni pa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama sheria ilivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha sisi watambikaji na Walawi pamoja na watu wote tukaipigia kura michango ya kuni, watakazoipelekea Nyumba ya Mungu wetu milango kwa milango ya baba zetu mwaka kwa mwaka penye siku zilizowekwa, tupate kuziteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)