Nehemiah 10:37 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila unga wetu wa kwanza, matoleo yetu, matunda ya miti, divai na mafuta tutavileta kwa kuhani kwenye vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Tena tutaleta zaka zetu za mazao yetu kwa Walawi, kwani ndio wanaohusika na ukusanyaji wa zaka hizo katika vijiji vyetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Zaidi ya hayo, tutaleta katika maghala ya nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila unga wetu wa kwanza, matoleo yetu, matunda ya miti, divai na mafuta tutavileta kwa kuhani kwenye vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Tena tutaleta zaka zetu za mazao yetu kwa Walawi, kwani ndio wanaohusika na ukusanyaji wa zaka hizo katika vijiji vyetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na matoleo yetu, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi ndio wanaozitwaa zaka vijijini kwetu kote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila unga wetu wa kwanza, matoleo yetu, matunda ya miti, divai na mafuta tutavileta kwa kuhani kwenye vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Tena tutaleta zaka zetu za mazao yetu kwa Walawi, kwani ndio wanaohusika na ukusanyaji wa zaka hizo katika vijiji vyetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena tukajisimamisha kutoa malimbuko ya unga wetu wa kwanza wa kupika mikate na michango mingine itupasayo na matunda ya miti yote na mvinyo mbichi na mafuta, tuyapelekee watambikaji katika vyumba vyao vilivyopo penye Nyumba ya Mungu wetu, nao Walawi tuwapelekee mafungu ya kumi ya mashamba yetu, kwani Walawi ndio wanaoyatoza mafungu ya kumi katika miji yote, tunakolima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)