Nehemiah 10:38 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani, mzawa wa Aroni, atakuwa na Walawi wanapopokea zaka. Halafu Walawi watapeleka sehemu ya kumi ya zaka zote zilizotolewa katika nyumba ya Mungu kwenye vyumba na ghala.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani aliye wa uzao wa Haruni atashirikiana na Walawi wanapopokea zaka. Nao Walawi watapaswa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika maghala ya hazina yaliyo katika nyumba ya Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani, mzawa wa Aroni, atakuwa na Walawi wanapopokea zaka. Halafu Walawi watapeleka sehemu ya kumi ya zaka zote zilizotolewa katika nyumba ya Mungu kwenye vyumba na ghala.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wapokeapo zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atokanaye na uzao wa Haruni atashirikiana na Walawi wakati wanapopokea zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani, mzawa wa Aroni, atakuwa na Walawi wanapopokea zaka. Halafu Walawi watapeleka sehemu ya kumi ya zaka zote zilizotolewa katika nyumba ya Mungu kwenye vyumba na ghala.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena Walawi wakiyatoza mafungu ya kumi, mtambikaji aliye mwana wa Haroni sharti awe pamoja na hao Walawi, Walawi wapeleke fungu la kumi la mafungu yao ya kumi vyumbani mwa nyumba ya vilimbiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.