Nehemiah 10:39 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa Israeli, pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala mahali vifaa vya mahali patakatifu vihifadhiwapo na wanapokaa makuhani wanaohudumu, mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani humo vyumbani ndimo, wana wa Isiraeli na wana wa Lawi watakamopeleka michango ya ngano na ya mvinyo mbichi na ya mafuta, kwani humo ndimo, vyombo vitakatifu vilimo, nao watambikaji na watumishi na walinda malango na waimbaji wamo mumo humo. Hatutaiacha Nyumba ya Mungu wetu, ikose cho chote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)